,

,

,

,
News

RC Makonda aagiza kubomolewa nyumba 36 bonde la Msimbazi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameagiza kubomolewa kwa nyumba 36 ambazo zipo kwenye maeneo hatarishi ya mabondeni ikiwemo bonde la mto Msimbazi, hali ambayo imepeleka kaya nyingi kukumbwa na mafuriko.
 
Makonda amezitembelea nyumba hizo katika Kata ya Bugurni kwa Mnyamani na Tabata , akiwa na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo ameshuhudia maafa makubwa yakiwemo ya baadhi ya watu kupoteza mali pamoja na nyumba zao kujaa maji.
Kufuatia mvua zilizoanza kunyesha tarehe nane mwezi huu, zimepelekea kuleta maafa ikiwemo kifo cha mtu mmoja kilichotokea eneno la Jangwani Jijini Dar Es Salaam, pamoja na watu wengi kupoteza makazi, jambo ambalo limemgusa RC Makonda na kufikia uamuzi huo wa kuiomba Halmashauri ya Ilala kuanza zoezi hilo la ubomoaji mara moja.
RC Makonda amesema kuna watu ambao tayari wamelipwa pesa kuhama maeneo hayo lakini cha ajabu wengine hawajaondoka na wengine wamewapangisha watu wengine kwenye maeneo hayo hatarishi, jambo ambalo serikali yake haiwezi kulikalia macho na kuagiza kubomolewa kwa nyumba hizo.
Pia amewataka wale ambao hawajahakiki taarifa zao kuhusu kupewa hifadhi baada ya nyumba zao kubomolewa wafanye hivyo kwa kwendaq ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa uhakiki huo

Jozey The Boy inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Instagram na Twitter ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment

copyright © 2016 Jozey The Boy. Powered by Blogger.