Mtayarishaji wa muziki kutoka ‘Wasafi Record’ Laizer amefunguka kwa kusema kuwa haoni kama Harmonize anaiga uimbaji wa Diamond kama baadhi ya watu wanavyodai.
Laizer ambaye ametengeneza hits kadhaa kama ‘Bado’ ya Harmonize na Diamond, ‘Salome’ ya Diamond pamoja na nyingine nyingi za wasanii wa WCB, amesema yeye kama producer anaona kila msanii anaimba katika mtindo wake.
“Binafsi mimi sioni kama Harmonize anaimba kama Diamond,” Laizer alikimbia kipindi cha FNL cha EATV. “Kwa sababu hata ukisikia ule wimbo ya ‘Bado’, bado utajua huyu ni Harmonize na yule ni Diamond. Pia labda ni kwa sababu wanaendana ndiyo maana wanafananishwa lakini kila mtu anaimba kivyake kabisa,”
Pia mtayarishaji huyo alisema kila msanii wa WCB ana upekee wake katika muziki wake
0 comments:
Post a Comment