Baadhi ya kundi la mabaharia wa
Kiasia walioachiwa na maharamia wa Kisomali baada ya kuwa matekani kwa
karibu miaka mitano wamezungumzia kuhusu mateso yao nchini kenya.
Mmoja wa mateka hao Arnel Balbero kutoka Ufilipino aliiambia BBC kuwa walikua wakipata mateso zaidi ya wanyama na ilibidi kuwinda panya kwa ajili ya chakula.Maharimia hao waliwakabidhi mabaharia hao 26 kwa mamlaka huko kaskazini mwa somalia katika mji Galkayo siku ya jumamosi asubuhi. waliwasili mji mkuu wa Kenya, Nairobi siku ya Jumapili.
Sasa wanarudi katika nchi zao huko China, Taiwan, Vietnam, Kambodia, Ufilipino na Indonesia. Mabaharia hao walitekwa mwaka 2012 wakati maharamia walipoteka mashua yao ya uvuvi karibu na ushelisheli.
0 comments:
Post a Comment