Uturuki imesema vikosi vyake
vilivyoko Iraq vimechukua hatua ya kujilinda dhidi ya kundi la kigaidi
la dola la kiislamu karibu na mji wa Mosul huko Iraq, lakini serikali
ya Iraq imekataa kuhusika kwake.
Kundi la Peshmerga limesema kuwa limekamata mji wa Bashiqa, ulioko kilomita kumi na mbili kutoka mji wa Mosul. Na Uturuki imesisitiza kuwa lazima itashiriki kulinda mji wa Mosul.
Waziri mkuu wa Iraqi Haider al-Abadi amekanusha madai hayo, japokuwa Marekani imeshauri kufanyika kwa makubaliano.
0 comments:
Post a Comment